Ujerumani itakuwa na timu nne katika kinyang'anyiro cha Champions League
katika awamu ya makundi inayoanza kesho Jumanne kwa mara ya kwanza , na
jibu la kwanza litapatikana mwishoni mwa mwaka huu wakati Bayern Munich
, Borussia Dortmund , Bayer Leverkusen na Schalke 04 ambazo zote
zinakwaana na timu kutoka Premier League zitakapoonesha matokeo yake.
Mlinzi wa zamani wa Leverpool Sami Hyypia anaoiongoza Bayer Leverkusen kesho katika kundi A ambapo inapambana na Manchester United, ambapo kocha wa zamani wa Everton David Moyes anafuata nyazo za Sir Alex Ferguson , ambaye aliiongoza timu hiyo katika mafanikio ya taji la Champions League mwaka 1999 na 2008.
Mlinzi wa zamani wa Leverpool Sami Hyypia anaoiongoza Bayer Leverkusen kesho katika kundi A ambapo inapambana na Manchester United, ambapo kocha wa zamani wa Everton David Moyes anafuata nyazo za Sir Alex Ferguson , ambaye aliiongoza timu hiyo katika mafanikio ya taji la Champions League mwaka 1999 na 2008.
Hyypia anadai kuwa haendi Old Traford kupata saini ya kumbukumbu ya Wayne Rooney , lakini kupata points za mwanzo katika kundi hilo ambalo pia lina timu za Real Sociadad na Shakhtar Donetsk.
Bayern inafungua kampeni yake ya kutetea taji lake na CSKA Moscow katika kundi D wakati Manchester City ambayo sasa inaongozwa na Manuel Pellegrini itakuwa katika jamhuri ya Czech kupambana na Viktoria Plzen.
Makamu bingwa Borussia Dortmund kabla ya kuchomoa upanga wake kupambana na Arsenal London , ina kibarua na Napoli siku ya Jumatano, timu ambayo pia ina kocha mpya ambaye aliwahi kuzifunza Liverpool na Chelsea , Rafael Benitez na pia mshambuliaji mpya kwa jina la Gonzalo Higuain.
Arsenal inafungua dimba kwa kupambana na Olympique Marseille.
Schalke 04 iko katika kundi E pamoja na Chelsea ya Jose Mourinho ambapo timu hiyo ya Ujerumani inafungua dimba na Steaua Bucharest, wakati Chelsea inamiadi na Basel ya Uswisi.
"La Decima"
Vigogo vya soka nchini Uhispania , Real Madrid na Barcelona sio tu kwamba wana makocha wapya , lakini pia wamesajili wachezaji ghali kabisa msimu huu Gareth Bale na Neymar.
Ushirikiano kati ya Ronaldo na Bale na Messi na Neymar utakuwa wa kuvutia machoni, wakati Real wanataka kwa udi na uvumba kupata taji lao la kumi, "La Decima", lakini matumizi ya zaidi ya euro milioni 600 katika misimu miwili iliyopita kununua wachezaji katika kikosi hicho yatakuwa kipimo iwapo hilo linaweza kutimia.
Bale amesema wakati akitambulishwa kwa klabu hiyo kuwa "Ninataka kuisaidia timu hii kupata "La Decima" , akimaanisha taji la kumi la Champions League kwa Real Madrid.
Real Madrid ina miadi na Galatasaray ya Uturuki kesho Jumanne katika kundi B ambalo pia lina timu za Juventus na Copenhagen.
Barca ambayo inakumbana na AC Milan kwa mwaka wa tatu mfululizo iko katika kundi C, na ainaanza na Ajax Amsterdam.
Paris St Germain ambayo itacheza kesho Jumanne katika kundi C inapambana na Olympiacos.
No comments:
Post a Comment