Mshindi wa tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka 2013, anatarajiwa kutangazwa Jumatatu, Desemba 2, 2013.
Mshindi huyo atatangazwa kwa wakati mmoja katika
redio na televisheni ya BBC, Focus on Africa, saa mbili na dakika 35
usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Idhaa ya Dunia ya BBC ilitangaza
orodha ya wachezaji kutoka Afrika watakaowania tuzo ya BBC ya mwanasoka
bora wa mwaka 2013 ijulikanayo kama "BBC African Footballer of the Year
award".
Wachezaji waliotajwa na wataalam wa masuala ya soka kuwania tuzo hiyo ni:
1.Pierre-Emerick Aubameyang - mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon na Borussia Dortmund ya Ujerumani.
2.Victor Moses - wa timu ya taifa ya Nigeria na Liverpool ya England akiwa katika mkopo kutoka timu ya Chelsea pia ya England.
3.John Obi Mikel - mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Chelsea ya England.
4.Jonathan Pitroipa -mchezaji wa Burkina Faso na Rennes ya Ufaransa.
5.Yaya Touré - mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na pia timu ya Manchester Cityya England.
Kazi ya kuwapigia kura wachezaji hao ilianza
tarehe 11 Novemba 2013 saa nane na dakika arobaini na tano kwa saa za
Afrika Mashariki, wakitangazwa katika kipindi cha asubuhi cha BBV cha
Newsday.
No comments:
Post a Comment