Joachim Low: Licha ya kuwafunga Brazil kwa mvua ya magoli sasa nahisi huruma
|
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amesema
pamoja na furaha iliyokithiri kambini kwake kufuatia matokeo ya kihistoria
waliyoyapata kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali usiku wa kuamkia hii leo,
bado anahisi huruma kwa wapinzani wao Brazil.
Low, amesema anajihisi huruma kutokana na wenyeji Brazil
kuambulia kibano ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya soka lao, hali
ambayo anadhani huenda ikawa ni zaidi ya maumivu kwa mashabiki nchini humo.
Amesema alijisi unyonge pale alipokutana na kila shabiki
ama afisa wa Brazil katika korido ya kuelekea kwenye vumba vya kubadilishia, na
yeye kama binaadam alingia huruma na kutamani kulia lakini ujasiri wa ushindi
mkubwa alioupata ulimpa nafasi ya kutembea kifua mbele.
|
No comments:
Post a Comment