Wachezaji wa Costa Rica wakipokewa kishujaa katika jiji la San Jose |
Licha ya kuwa katika kundi moja na vigogo vya soka ulimwengu katika kombe la dunia England, Italy
na Uruguay, hakuna mtu aliyeipa nafasi Costa Rica ya kufanya vizuri katika kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Lakini nchi hiyo ya Marekani ya kusini iliwashangaza wengi kufuatia kusonga mbele na kuingia hatua ya mtoano ya 16 bora na hata kusogea mpaka hatua ya robo fainali na kwa bahati mbaya ikaondolewa kwa shida na Uholanzi kwa njia ya penati.
Timu hiyo haikufungwa ndani ya dakika 90 katika michezo yote ambapo kikosi hicho kiliendelea kuonyesha ushujaa kiasi kupokelewa kishujaa waliporejea nchini Costa Rica.
Baada ya kutua jijini San Jose, mji mkuu wa nchi hiyo kikosi hicho kilijikuta kikizingirwa na mashabiki wa nchi hiyo na kufanya sherehe ya kuzunguka mtaani huku kila mtu akijitokeza kuwasabahi wachezaji na maafisa wa timu hiyo.
Siyo mbaya, kwa nchi yenye watu milioni nne na nusu ambayo ni nusu tu ya idadi ya wakazi wa jiji la London.
No comments:
Post a Comment