Kiungo wa
kimataifa wa Mali Seydou Keita ameondoka Barcelona baada ya kuwepo katika klabu
hiyo katika kipindi cha mafanikio cha mataji lukuki ndani ya kipindi cha miaka
minne ya utumishi wake ndani ya klabu hiyo.
Barcelona
imetoa taarifa inayosomeka
"Seydou
Keita ametangaza usiku huu hataendelea na klabu hii msimu ujao,".
"Barcelona
inamshukuru Seydou Keita kwa mchango wake kwa miaka michache na inamtakia kila
la kheri zaidi katika soka lake kama professional
na mafanikio binafsi siku za baadaye."
Keita ambaye
amefanikiwa kutwaa mataji 14 akiwa na Barca anahusishwa na kutaka kuelekea
Uchina katika klabu ya Dalian Aerbin.
REKODI YA KEITA YA MATAJI BARCA
3 x Spanish league (2009, 2010, 2011)
2 x Uefa Champions League (2009, 2011)
2 x Copa del Rey title (2009, 2012)
2 x Fifa Club World Cup (2009, 2011)
2 x Uefa Super Cup (2009, 2011)
3 x Spanish Super Cup (2009, 2010, 2011)
Safari ya
wanasoka waafrika kuelekea Uchina imekuwa ikivuta nyota wengi ambapo sasa
tayari Didier Drogba, Frederic Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wote wamejiunga
vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Uchina maarufu kama Chinese Super League.
Keita mwenye
umri wa miaka 32 alijiunga Barcelona akitokea Sevilla mwaka 2008 na alikuwa ni
mchezaji wa kwanza kusainishwa na aliyekuwa kocha wakati huo baada ya kujiunga
na Barca Pep Guardiola.
Taarifa toka
Hispania zinasema Keita amekatisha mkataba wake ambao ulikuwa umalizike 2014 na
ambao ungemruhusu kuondoka kama mchezaji huru.
Huko nyuma
Keita kavitumikia vilabu kama Marseille, Lorient na Lens vyote vya nchini
Ufaransa kabla yan kujiunga na Seville kwa msimu mmoja.
No comments:
Post a Comment