Meneja wa
mashetani wekundu Manchester United Sir Alex Ferguson ametoa kali ya mwaka
baada ya kusema kuwa itakapo tokea timu yake kuzawadiwa penati basi atakwenda
kupiga yeye mwenyewe hii ni baada ya mshambuliaji wake Wayne Rooney kukosa
penati katika mchezo ambapo United iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal
jumamosi.
Mabao ya Robin
van Persie na Patrice Evra yalitosha kuwafanya mashetani wekundu kuzoa alama
zote tatu muhimu katika mchezo huo na kujikita katika kilele cha msimamo wa
ligi kuu ya England ‘Premier League’ kwa mara ya kwanza msimu huu.
Hata hivyo
ushindi wa mabao hayo 2-1 ungekuwa mkubwa zaidi andapo Rooney angefanikiwa
kufunga penati yake ambayo ilitoka nje penati ambayo ilitokana na Santi Cazorla
kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Rooney
amekuwa ni mchezaji wa nne wa United kukosa penati msimu huu ambapo meneja wake
mzee Alex Ferguson mwenye umri wa miaka 70 amekuwa akijiuliza nani mwingine
atakayepiga penati.
Katika hali
ya utani mzee huyo akiongea na The Sun akasema
"Nadhani
nitapiga mwenyewe wiki ijayo na nitafunga”.
Van Persie,
Javier Hernandez na Luis Nani ni miongoni mwa wachezaji wengine waliokwisha
kukosa penati msimu huu lakini Rooney anasema matokeo ya mchezo huo ndio
yaliyokuwa muhimu zaidi.
“haya mambo
huwa yanatokea na yamekwisha sasa".
“ki ukweli
nilihuzunika lakini ninasonga mbele na kwa kuwa tulishinda mchezo nadhani hilo
lilikuwa muhimu zaidi.”
QPR haistahili kuwepo chini katika
msimamo wa ligi anasema Cisse.
Mshambuliaji
wa QPR Djibril Cisse amesema timu yake ina ubora na nzuri licha ya kushindwa
kushinda katika jumla ya michezo ya 10 ya ligi msimu huu na jana kwenda sare ya
bao 1-1 kule Loftus Road dhidi ya Reading.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa wa Ufaransa alifunga goli la kusawazisha kwa wenyeji hao
wa mchezo huo wa jana katika kipindi cha pili ambapo waliutawala mchezo licha
ya kushinda kuibuka na ushindi na ambapo wamejiweka katika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi juu ya Southampton
kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 31 amesisitiza kuwa kikosi chake kina ubora wa kuweza
kupanda juu katika msimamo wa ligi kuu ya England na kuepuka kuwepo katika eneo
la hatari lakini pia akisema wanapaswa kusahau majina na kuongea na kuanza
kumalizia nafasi wanazotengeneza za ufungaji ili kujinasua na kuwa salama.
Amenukuliwa Sky
Sports akisema,
"tulikuwa
na fursa ya kushinda. Kama unapata nafasi ya wazi ya kufunga unapaswa kufunga. Hicho
ndicho tunachokikosa kwasasa lakini tunaendelea kujaribu"
"ubora tulionao katika timu
hatustahili kuwepo chini katika msimamo, hatuheshimiwi na timu nyingine lakini
hatustahili kuwepo pale.
"mpira
unachezwa uwanjani na si majina au kuongea. Tunapaswa kufanya hivyo kila mchezo."
Manchester City haija iva kutwaa tali
la ligi ya mabingfwa ulaya anasema Mancini.
Meneja wa Manchester
City Roberto Mancini amesema ni wazi itawawia vigumu sana safari hii kwa timu yake
kufuzu kutoka katika hatua ya makundi ya michuano ya vilabu bingwa Ulaya mwaka huu.
Mabingwa hao
wa ligi kuu ya England kwasasa wako mkiano katika kundi lao, kundi ambalo
linaonekana kuwa gumu kwao baada ya kupoteza kwa Real Madrid na Ajax kisha kupata sare dhidi ya Borussia Dortmund.
Wakati nafasi
ya kufuzu ikiwa finyu kwao meneja huyo mwenye umri wa miaka 47 amekiri kuwa bado
haamini kama kikosi chake kama kweli kiko katika uwezo wa kimashindano katika
michuano hiyo.
Akiongea na
Guardian amenukuliwa akisema,
"sidhani
kama tuko tayari kushinda taji la vilabu bingwa safari hii".
"kama
tunasema tuko tayari basi haitoki moyoni. Katika michuano hii matokeo ya
kushangaza yanaweza kutokea mwezi Februari na Machi lakini ni kwamba pia tuko
katika kundi gumu mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka jana.
"sisi
ni timu nzuri lakini hatuko tayari kwa michuano hii kama ilivyo kwa timu
nyingine. Chelsea ilijaribu kwa miaka 10 kushinda taji. Bila shaka ilikuwa timu
bora ulaya mwezi May baada ya miaka 10 pengine walistahili. Walistahili kushinda
miaka mitatu au minne iliyopita."
Licha ya
ugumu huo ulio mbele yao, bado Mancini na kundi lake wanategemea kusonga mbele
kusaka alama tisa muhimu katika jumla ya michezo iliyosalia.
No comments:
Post a Comment