KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, November 4, 2012

KUTOKA MORO NEWS BLOG: NGASSA AKINUKISHA SIMBA AWATUPIA JEZI APEWA YA YANGA AONDOKA KIVYAKE REDONDO, KAZIMOTO NAO WAMUUNGA MKONO.

Ngassa akitoka uwanjani akisindikizwa na mashabiki wa yanga
 
  Wachezaji watatu Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto na Ramadhani Chombo "Redondo" wa Simba wamezira na kuondoka kila mtu kivyake baada ya kichapo kutoka kwa Mtibwa sugar cha mabao 2-0.
 
 Kazimoto ndio alikuwa wa kwanza kutoka baada ya mpira kumalizika aliingia vyumbani nakubadilisha jezi na kutoka nje ambapo alichukua tax nakuondoka uwanjani.
 
 Baada ya mda kidogo ikatokea purukushani ndani ya basi la Simba na muda mfupi Ngassa na Redondo walishuka nakuondoka.
 
 Ngassa aliposhuka alitoa jezi yake aliyokuwa ameweka kwenye begi lake nakuirusha ndani ya basi hilo nakuondoka huku akishangiliwa na mashabiki wa Yanga huku wakiimba Ngassa rudi nyumbani na kumkabidhi jezi ya Yanga huku wakielekea kituo cha polisi. 
 
Alipofika Polisi MoroNew Blog ilizungumza nao na akajibu "majungu kaka" hata hivyo tulipo wadadisi zaidi tax ilifika nawao kuondokaa.
 
Wachezaji wengine wote waliondoka na basi kama kawaida huku basi hilo likisindikizwa na polisi kuzuia mashabiki watimu hiyo waliokuwa na hasira kali wasifanye vurugu.
 
  Washabiki wengi wamekuwa wakimlaumu kaseja kwa kusababisha goli la kizimbe huku wengine wakilalamika kwa kudai kumuona kaseja club moja ya usiku hapa mjini Morogoro inayo fahamika zaidi kwa jina four Star usiku wa kuamkia leo siku ya mechi.

No comments:

Post a Comment