Uongozi wa
klabu bingwa Tanzania Bara Simba ya mtaa wa Msimbazi umeamua kufutilia mbali
kamati zake zote kwa lengo la kujipanga upya kwa ajili ya ligi kuu ya soka
Tanzania Bara pamoja na michuano klabu bingwa barani Afrika.
Kauli ya
kuvunja kamati hizo imetolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo alhaji Ismail Aden Rage(mbunge) katika mkutano
wake na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo Kariakoo
mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Rage ambaye
hata hivyo hakutaja ni lini kamati mpya zitaundwa, pia amekiri kuwa matokeo ya
michezo ya mwisho ya timu yao hayakuwa mazuri kiasi cha kuwasikitisha wanachama
na wapenzi wa klabu yao.
Amesema mfululizo wa
kuendelea kuharibu kulitokana na wachezaji wa timu hiyo kuharibikiwa
kisaikolojia na kwamba ili kuhakikisha hali hiyo inaondoka katika vichwa vya
wameamua kuitoa timu yao nje ya nchi katika kujaribu kuwarejesha mashindanoni
ambapo ameahidi kutanga nchi hiyo baadaye.
Amewataka wanachama
na wapenzi wa Simba kufahamu kuwa katika kipindi hiki ligi ya Tanzania bara
imekuwa katika ushindani mkubwa hivyo ni vema wakawa wavumilivu na hali hiyo
tofauti na ilivyoljitokeza katika siku za hivi karibuni ambapo kikundi cha wanachama
kimoja kiliibuka na kutaka kuhatarisha hali ya amani ya klabu yao.
Pia Rage
ametangaza kulifuta tawi la Simba la Mpira pesa ambalo uongozi wa Simba umesema
lilichochea vurugu za hivi karibuni ambapo pia Rage ametangaza kumfuta
uanachama mwenyekiti wake Masoud Awadhi kwa kuitisha kikao batili cha wanachama
pia kutokana na kutokulipa ada ya uanachama kwa miaka mitatu.
Novemba 5 kuliibuka tafrani katika makao makuu ya klabu hiyo ambapo wanachama wa tawi la mpira pesa na baadhi ya wapenzi wa timu waliutaka uongozi wa juu wa klabu hiyo kuondoka na kuwaachia simba yao.
Mbango yalisomekam "Kaburu na Kaseja ondokeni tuachieni Simba yetu" jambo lilionekana kama vurugu zimeanza msimbazi lakini jitihada za msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga kuwatuliza wanachama zilizaa matunda kwa kujibu hoja mbalimbali za wanachama zilizoibuka kupitia vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment