Roy Keane amemshutumu Sir Alex Ferguson kwa kuwa ‘massive
ego’ na anaamini kuwa meneja wake huyo wa zamani bado anajaribu kuisimamia Manchester United licha ya kujiweka pembeni mwishoni mwa msimu uliopita.
Kocha huyo wa Ireland ameanzisha tena vita ya maneno kwa mara nyingine tena dhidi ya bosi wake wa zamani katika mahojiano ya television ambayo inaarifiwa kuwa yataonyeshwa Kesho usiku ambayo yatakuwa na mambo mengi toka kwa Kean akimuelezea Ferguson kama mtu ambaye hana maana na hana uadilifu.
Wawili hao walianza kuingia katika mvutano mwaka 2005 kufuatia Keane kuhojiwa televisheni ya klabu hiyo ambapo kwa nguvu zote aliwakosoa wachezaji wenzake.
Kiungo huyo aliondoka ndani ya klabu hiyo muda mfupi baadaye ambapo alieleza kuwa mahusiano yake na Ferguson hayakuwa mazuri tena.
Keane ametanabaisha kuwa ameanza kuangalia michezo ya United baada ya kuondoka kwa Ferguson lakini mzee huyo ana nguvu ndani ya klabu hiyo akiwa na nafasi ya ukurugenzi na anapigana kusamama dhidi ya David Moyes.
Kila kitu ni nguvu ya uendeshaji na kusimamia, bado anapigana licha ya kwamba sio meneja. Kean alikuwa akiongea na ITV4 na makala hiyo imepewa jina la ‘Keane and Vieira: The Best of Enemies’.
‘There’s massive ego involved in that.’
Furguson alimkosoa vikali Kean kupitia autobiography yake aliyoitoa hivi karibuni lakini raia huyo wa Ireland alichukuwa hiyo kama ujiko aliopewa na bosi wake wa zamani .
Furguson alimkosoa vikali Kean kupitia autobiography yake aliyoitoa hivi karibuni lakini raia huyo wa Ireland alichukuwa hiyo kama ujiko aliopewa na bosi wake wa zamani .
No comments:
Post a Comment