Hussein Sharifu wa Mtbwa atua Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili
|
Mlinda mlango Husein Sharif maarufu kama Casillas (Pichani juu akiwa na Kocha wa makipa wa Taifa Stars Juma Pondamali) amejiunga na klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea kwa wakata miwa wa Mtibwa Sugar ya Morogoro. Mlinda mlango huyo ambaye alikuwa ngome kubwa ya milingoti mitatu ya watoto wa Manungu Turiani , amekwenda kuchukua nafasi iliyo achwa wazi na mlinda mlango raia wa Ghana Yaw Berko aliyemaliza mkataba wake na wekundu hao wa Msimbazi. Taarifa za kukamilika kwa usajili wa mlinda mlango huyo pamoja na wachezaji wengine wawili vijana Manyika Opeter na Ibrahim Hajibu zimethibitishwa na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu mchana wa leo. |
No comments:
Post a Comment