Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeiomba kampuni ya bia
nchini TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt kuendelea kuidhamini ligi kuu ya
soka visiwani humo kwa lengo la kuendeleza dhana ya kutoa ajira kwa vijana
kupitia medani ya soka.
Waziri wa habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh Said Ally
Mbaruk amesema tangu TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt walipokubalia
kuidhamini ligi ya ZFA, kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa vijana ambao
kutokana na kuonyesha nia ya kutaka kujikita katika michezo hususana mchezo wa
soka halia mbayo anaamini itaendelea kuisaidia serikali ya SMZ kutatua tatizo
la ajira.
Said Ally Mbaruk amesema kampuni hiyo pia imeongeza chachu
katika wigo wa kuundwa kwa timu ya taifa ya Tanzania ambapo kwa sasa wachezaji
wengi wanaoitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars wanatoka visiwani Zanzibar.
Kwa msimu wa mwaka 2014-15 kampuni ya bia nchini TBL
kupitia kinywaji cha Grand Malt imesaini mkataba wa kuidhamini ligi ya visiwani
Zanzibar wa shilingi 244 tofauti na msimu uliopita ambapo kiasi cha fedha
kilikuwa ni shilingi million 204.
No comments:
Post a Comment