Kocha mkuu wa Simba Logarocic na msaidizi wake Matola |
Uongozi wa vilabu vya vinavyo shiriki ligi kuu ya Soka Tanzania Bara vya Mtibwa Sukari na Simba SC vimesikitishwa na maamuzi yaliyochukuliwa
na shirikisho la soka nchini TFF ya kusogeza mbele tarehe ya kuanza kwa ligi kuu ya
soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014-15.
Afisa habari wa klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Manungu,
Turiani mkoani Morogoro Thobias Kifaru amesema hatua hiyo ya TFF haikufuata nidhamu ya kiufundi na kimashindano hata kidogo na kwamba viongozi wa TFF walipaswa
kufanya maamuzi hayo kwa kuwashirikisha viongozi wa klabu za ligi kuu, kwa
ajili ya kupata muafaka wa pamoja.
Kifaru amesema wakati kama huu wa maandalizi ya msimu mipango ya makocha wote huwa inaendana na Programu zao kwa mujibu wa kalenda huku pia suala la kiuchumi katika kuviweka vilabu hivyo kambini pia linaendana na kalenda hivyo kufanya maamuzi kama hayo ni kuharibu mipango hiyo kwa pamoja.
Amesema TFF wamekuwa wakifanya maamuzi kama hayo kila
mara pasina kuzingatia hasara kubwa ambazo zimekua zikizikabili klabu za ligi
kuu ambazo zinatumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya maandalizi.
Kikosi cha Mtibwa Sugar ya Morogoro |
Kwa upande wa Wekundu wa Msimbazi Simba kupitia kwa afisa habari wake Asha Muhaji amesema licha ya kikosi
chao kuanza mazoezi ya Gym hapo jana bado kusogezwa mbele kwa tarehe ya kuanza kwa
ligi kuu kutoka Agosti 24 mpaka Septemba 20 kumewaathiri kwa kiasi fulani mipango yao ya maandalizi kwa ujumla kwa kuwa ratiba hiyo mpya inapangua mipango waliyokuwa
wameiiwekea kabla ya kuanza rasmi kambi yao.
Muhaji amesema
kuharibika kwa mipango hiyo kwa sasa, kunatoa changamoto mpya viongozi
walioingia madarakani mwishoni mwa mwezi uliopita kujipanga tena na maandalizi yao kutegemeana na maoni ya mwalimu wao Mcroatia Zdravko Logarusic ambaye alikuwa akitarajiwa kurejea nchini hii leo.
No comments:
Post a Comment